WIGAN ATHLETIC YAMTANGAZA GARY CALDWELL KAMA MENEJA MPYA WA TIMU HIYO

WIGAN ATHLETIC YAMTANGAZA GARY CALDWELL KAMA MENEJA MPYA WA TIMU HIYO

Like
275
0
Wednesday, 08 April 2015
Slider

Timu ya Wigan Athletic imemtangaza Gary Caldwell kuwa meneja wao mpya akirithi mikoba ya Malky Mackay aliyetimuliwa mapema jumatatu.

Mackay kibarua cha kuinoa klabu hiyo kiliota nyasi kufuatia kichapo cha 2-0 dhidi ya Derby katika uwanja wa nyumbani

Caldwell aliyekuwa mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Scotland mwenye umri wa miaka 32, ameichezea Wigan michezo 111 lakini pia alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha timu hiyo kilichotwaa kombe la FA mwaka 2013.

Caldwell alitangaza kustaafu mapema kwenye msimu huu kufuatia maumivu ya mara kwa mara kwenye maungio ya mguu.

Kwa nafasi hiyo ya Caldwell ni meneja wa tatu kwa msimu huu

Comments are closed.