WITO UMETOLEWA KWA MASHIRIKA, MAKAMPUNI NA TAASISI KUSAIDIA JAMII

WITO UMETOLEWA KWA MASHIRIKA, MAKAMPUNI NA TAASISI KUSAIDIA JAMII

Like
444
0
Monday, 28 September 2015
Local News

WITO umetolewa kwa Taasisi, mashirika na makampuni kote nchini kujenga utamaduni  wa kutumia sehemu ya faida wanayoipata kuisaidia jamii kupitia sekta ya afya ambayo inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Wito huo umetolewa mjini Kisarawe na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Profesa Emanueli Mjema wakati akikabidhi msaada wa mashuka 176 yaliyotolewa na chuo hicho kusaidia wodi ya Wazazi ya Hospitali ya wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.

Amesema chuo cha CBE mwaka huu kimetimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1965, hivyo ukongwe na umri wake nchini umekuwa ukiendana na mabadiliko ya kiuchumi  yanayotokea ndani na nje ya nchi ili kukidhi mahitaji na matarajio ya watanzania.

1203

 

4101

Comments are closed.