WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO YAKUSUDIA KUTOA TAARIFA YA WANAWAKE WANAOFARIKI KWA MATATIZO YA UZAZI

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO YAKUSUDIA KUTOA TAARIFA YA WANAWAKE WANAOFARIKI KWA MATATIZO YA UZAZI

Like
302
0
Friday, 06 May 2016
Local News

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa inakusudia kutoa taarifa ya wanawake wanaofariki Dunia kutokana na matatizo ya uzazi kila baada ya miezi mitatu ili kukabiliana na tatizo la vifo vya wanawake nchini.

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Viongozi Wanawake kuhusu masuala ya Afya.

 

Ameeleza kuwa, katika uteuzi atakaoufanya kwenye bodi zilizo chini ya Wizara yake, atahakikisha asilimia 30 ya wajumbe wa bodi hizo ni wanawake.

Comments are closed.