WIZARA YA AFYA YAKANUSHA UWEPO WA EBOLA

WIZARA YA AFYA YAKANUSHA UWEPO WA EBOLA

Like
238
0
Wednesday, 12 August 2015
Local News

WIZARA ya afya na ustawi wa jamii imesema kuwa mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote juu ya kifo cha mgonjwa mwenye umri wa miaka 39 kutoka katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma ambacho kimetokana na ugonjwa wa Ebola.

Taarifa ya ufafanuzi iliyotolewa na kitengo cha awasiliano kutoka wizarani hapo imeelezwa kuwa sampuli ya mgonjwa huyo imechukuliwa na kupelekwa kwenye maabara ya taifa ya jamii wizara ya afya kwa uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo cha ugonjwa huo.

Comments are closed.