SERIKALI kupitia Wizara ya Fedha imewasilisha Muswada wa sheria ya mfumo wa malipo ya Taifa ya mwaka 2015 wenye lengo la kuzuia, kuimarisha na kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza katika mfumo wa malipo uliopo.
Akiwasilisha rasmi muswada huo leo Bungeni mjini Dodoma waziri wa Fedha mheshimiwa SAADA MKUYA amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuiweka nchi katika mazingira ya ushindani wa kibiashara na kutengeneza ufanisi mkubwa wa malipo.
Mbali na hayo waziri MKUYA ameeleza kuwa katika kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa ubora unaotakiwa serikali imeweka utaratibu wa kutambua nyenzo za kielektroniki za ulipaji wa malipo pamoja na utoaji wa leseni kupitia huduma hiyo.