WIZARA YA MAJI NA JESHI LA POLISI LAFANYA KAMPENI KUSAKA WAHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA MAJI KINONDONI

WIZARA YA MAJI NA JESHI LA POLISI LAFANYA KAMPENI KUSAKA WAHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA MAJI KINONDONI

Like
267
0
Friday, 13 March 2015
Local News

WIZARA ya maji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni imefanya Operesheni ya kukamata wezi wanaoiba  Miundo mbinu ya maji ili kuondoa kero ya upatikanaji wa maji katika sehemu mbalimbali jijini dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  PAUL MAKONDA amesema kuwa, katika oparesheni hiyoWilaya ya Kinondoni ni mojawapo ya wilaya ya Mkoa wa Dar es salaam zilizohujumiwa na kuwa na wizi mkubwa wa maji katika miundo mbinu yake.

Aidha  amesema kuwa gharama za maji zinapanda kutokana na watu wachache wanaoiba maji hivyo amewataka wananchi kutowafumbia macho wahalifu hao kwani kwa kufanya hivyo bei ya huduma za maji itashuka tofauti na ilivyo sasa.

Comments are closed.