WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAAJIRI WATUMISHI WAPYA 588

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAAJIRI WATUMISHI WAPYA 588

Like
286
0
Thursday, 29 October 2015
Local News

WIZARA ya Maliasili na Utalii imefanikiwa kutoa ajira mpya kwa Watumishi wapya 588 katika kitengo cha Afisa Wanyamapori na Wahifadhi wanyamapori lengo ikiwa ni kukabiliana na tatizo la kuenea kwa vitendo vya ujangili kwa wanyama.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo elekezi kwa waajiriwa hao jana katika Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Temeke jijini Dar es Salam, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, dokta Adelhelm Meru amewashauri watumishi kujituma zaidi ili kukidhi malengo yaliyowekwa.

Mbali na hayo amewataka Watumishi hao kujiepusha na tabia ya kupokea rushwa hasa kwa watumishi waliopo kwenye Mapori ya akiba, mapori tengefu na vituo vingine vya kazi kwani atakayethibitika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Comments are closed.