WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATANGAZA UGUNDUZI WA GESI ASILIA KWENYE BAHARI KUU YA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATANGAZA UGUNDUZI WA GESI ASILIA KWENYE BAHARI KUU YA TANZANIA

Like
347
0
Tuesday, 31 March 2015
Local News

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetangaza ugunduzi wa Gesi Asilia katika Miamba ya Mchanga kwenye Kisima kinachochimbwa na Statoil cha Mdalasini-1 kwenye Bahari Kuu ya Tanzania.

Waziri wa Nishati na Madini, GEORGE SIMBACHAWENE amebainisha hayo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma baada ya kuthibitishwa na Makamu wa Rais wa Statoil, NICK MADEN pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania -TPDC.

Statoil ni Mkandalasi katika Leseni ya Utafutaji ya Kitalu namba 2 kwa niaba ya TPDC na inayohisa ya asilimia 65% na mshirika wake EXXONMOBIL and PRODUCTION Tanzania Limited inazo hisa asilimia 35.

Comments are closed.