WIZARA YA ULINZI URUSI YAKANUSHA KUANGUSHA MAKOMBORA IRAN

WIZARA YA ULINZI URUSI YAKANUSHA KUANGUSHA MAKOMBORA IRAN

Like
306
0
Friday, 09 October 2015
Global News

WIZARA ya ulinzi ya Urusi imekanusha madai yaliyotolewa na afisa mmoja wa Marekani kuwa makombora manne ya Urusi yaliyofyatuliwa katika Bahari ya Caspian kuelekea Syria yalianguka nchini Iran.

Msemaji wa wizara hiyo Jenerali Igor Konashenkov amesema makombora yote yaliyofyatuliwa yalipiga katika maeneo yaliyolengwa.

Afisa wa Marekani, ambaye jina lake halikujulikana, amesema makombora hayo yalianguka nchini Iran siku ya Jumatano lakini hakutoa maelezo yoyote kuhusu mahali yalikoanguka au ikiwa yalisababisha uharibifu wowote.

 

Comments are closed.