IMEELEZWA kuwa aliyekuwa kiongozi wa kidini wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda Osama Bin Laden aliacha urathi wa dola milioni 29 za kulifadhili kundi la Jihad kabla ya kuuawa mwaka 2011.
Kwa mujibu wa wosia wake aliouandika ambao umeonekana leo ameihimiza familia yake kuheshimu wosia wake na kuwashauri watumie mali yake yote kuendeleza kundi la jihad.
Mali yake na wasia wake ni miongoni mwa maelfu ya stakabadhi muhimu zilizofichuliwa leo na maafisa usalama wa Marekani ambao pia wosia huo umemtaka baba yake amtunzie mke na wanawe baada ya yeye kuaga dunia.