WZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI 2 CHATO

WZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI 2 CHATO

Like
432
0
Thursday, 17 March 2016
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa tuhuma za ubadhirifu, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

 

Watumishi hao ni Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika, bwana Mwita Mirumbe Waryuba pamoja na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya, Dioniz Mutayoba.

 

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana usiku alipokuwa akizungumza na watumishi wa idara zote na taasisi zilizomo kwenye wilaya ya Chato katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mshikamano SACCOS wilayani humo.

                                      

Comments are closed.