YANGA KILELENI MSIMAMO WA LIGI KUU

YANGA KILELENI MSIMAMO WA LIGI KUU

Like
317
0
Thursday, 19 March 2015
Slider

Yanga kinara msimamo wa ligi kuu Tanzania bara, katika mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa taifa jijini Daresalaam klabu ya soka ya Yanga ilikuwan mwenyeji wa Kagera Sugar ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Simon Msuva kwa mkwaju wa penati mnamo dakika ya nane baada ya kufanyiwa madhambi na mchezaji wa Kagera Benjamin Asukile, katika dakika ya 15 Hamisi Tambwe aliiandikia Yanga bao la pili magoli yaliyoifanya klabu hiyo kurejea kileleni na kuwa kinara wa ligi kuu.

Goli la Kagera lilifungwa na mchezaji Salum Kanoni kwa mkwaju wa penati.

Katika michezo mingine ya ligi kuu iliyochezwa hapo jana Simba sc ilipokea kichapo cha mgoli 2-0 kutoka kwa Mgambo Shooting kwenye uwanja wa Mkwakwani huko Tanga.

Kipigo hicho kinaweka Simba katika wakati mgumu kutwaa ubingwa lakini pia kukamata nafasi ya pili ya ligi.

Huko Shinyanga pia Katika mchezo ulioikutanisha Mbeya City na Stand Untd klabu ya soka yenye makazi yake jijini Mbeya iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwa bila.

Ushindi huo wa Mbeya City unaipa timu hiyo pointi 24 kwenye msimamo wa ligi huku Stand Untd wakiwa na pointi 22

Comments are closed.