YANGA USO KWA USO NA ETOILE DU SAHEL

YANGA USO KWA USO NA ETOILE DU SAHEL

Like
281
0
Tuesday, 07 April 2015
Slider

Yanga kushuka dimbani kumenyana na Etoile du Sahel ya Tunisia katika raundi ya pili ya michuano ya vilabu ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Yanga ambayo inaiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo imefanikiwa kuwatoa Platinum FC licha ya kufungwa 1-0 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Bulawayo, nchini Zimbabwe. Hii inafuatia ushindi wa 5-1 ambao Yanga iliupta katika mechi ya kwanza iliyochezwa hapa Dar es Salaam.

Yanga watakuwa na kazi ya ziada kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya Tanzania kufuatia rekodi ya klabu ya Etoile du Sahel kuwa na uzoefu wa kucheza michuano mikubwa Afrika, klabu hiyo imepata nafasi ya kukutana na Yanga baada ya kutoka sare ya 1-1 na timu ya Benfica de Luanda ya Angola. Katika mechi ya kwanza, Watunisia walishinda 1-0.

 

Comments are closed.