YAYA TOURE ANYAKUA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA KWA MARA YA NNE MFULULIZO

YAYA TOURE ANYAKUA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA KWA MARA YA NNE MFULULIZO

Like
276
0
Friday, 09 January 2015
Slider

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Manchester City, Yaya Toure afanikiwa kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa bara la Afrika kwa mara ya nne mfululizo.

Tuzo hiyo inayotolewa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF), imeshuhudia Yaya Toure akiwapiku wachezaji wawili, Pierre Emerick Aubameyang (Gabon) na golikipa wa timu ya taifa ya Nigeria, Vicent Enyeama.

Yaya alipata kura 175 dhidi ya mshambuliaji wa klabu ya Borrusia Dortmund, Aubemayang aliyejinyakulia kura 12o huku Enyeama akiangukia nafasi ya tatu kwa kupata jumla ya kura 105.

Katika hatua nyengine tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kutoka katika ligi za ndani imekwenda kwaFirmin Mubele Ndombe wa AS Vita huku ile ya mchezaji bora wa kike akinyakuliwa na Asisat Oshoala anayekigika katika klabu ya River Angels.

Comments are closed.