YEMEN: SHAMBULIO LA NDEGE LAUA 131

YEMEN: SHAMBULIO LA NDEGE LAUA 131

Like
212
0
Tuesday, 29 September 2015
Global News

IDADI  ya  watu  waliouwawa  katika  shambulio  la  anga kwenye  sherehe  ya  harusi  nchini  Yemen  imefikia  watu 131, na kuaminika kuwa  shambulio  hilo ni baya kuwahi kutokea  katika  vita  nchini Yemen.

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia ambao unafanya  mashambulizi  ya  anga  dhidi  ya  maeneo  ya waasi  nchini  Yemen  umekanusha kuhusika  na shambulio  hilo  huku msemaji wa  muungano huo amesema wanamgambo wa  eneo hilo huenda wameshambulia  kwa  makombora.

makombora  hayo yaliyorushwa jana yameharibu  mahema  katika  kijiji  cha  Al-Wahijah  katika bahari  ya  Sham, karibu  na  mji  wa  bandari  wa Al-Mokha ambapo  mtu  mmoja  anayehusika  na  kundi  la Wahuthi  alikuwa  akisherehekea harusi.

Comments are closed.