SERIKALI ya Yemen iliyo uhamishoni nchini Saudi Arabia imesema viongozi wa ngazi ya juu wa kundi la waasi wa Houthi wanafanya mazungumzo na maafisa wa Marekani nchini Oman kuendeleza juhudi za kuutafutia ufumbuzi mzozo wa Yemen.
Muungano unaongozwa na Saudi Arabia ulianza mashambulizi ya kutokea angani mwezi Machi mwaka huu katika harakati ya kumrejesha madarakani rais wa Yemen Abd-Rabbu Mansour Hadi.
Hadi alikimbia baada ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran kuudhibiti mji mkuu Sanaa mwezi Septemba mwaka uliopita na baadaye kuelekea maeneo ya katikati na kusini mwa nchi hiyo.