YEMEN YAOMBA MSAADA WA KIJESHI KUPAMBANA NA WAPIGANAJI WA KIHOUTHI

YEMEN YAOMBA MSAADA WA KIJESHI KUPAMBANA NA WAPIGANAJI WA KIHOUTHI

Like
304
0
Tuesday, 24 March 2015
Global News

WAZIRI wa Mambo ya nchi za Nje wa Yemen RIYADH YASEEN amezitolea wito nchi ya Ghuba ya Uarabu kuingilia Kijeshi katika nchi yake, kuwazuia wapiganaji wa Kihouthi ambao wanaipinga Serikali ya Rais ABDU RABBU MANSOUR HADI, ili wasiendeleei kuyateka maeneo zaidi ya nchi.

Katika mahojiano na Gazeti la Kiarabu la Al-Sharq al-awsat, Waziri YASEEN amesema wapiganaji hao wameteka Miji na Viwanja vya ndege, na kumtia kizuizini yoyote wanayemtaka.

Amesema wameelezea hofu yao kwa Baraza la Ushirikiano wa nchi za Ghuba, Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kimataifa, wakitaka liundwe eneo nchini humo ambamo ndege haziruhusiwi kuruka.

Comments are closed.