ZAHANATI YA DA.MA AFRICA YAZINDULIWA KIBAHA

ZAHANATI YA DA.MA AFRICA YAZINDULIWA KIBAHA

Like
304
0
Monday, 03 August 2015
Local News

MGANGA Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dokta. Happniness Ndosi amepongeza shirika la masisita Waabuduo Damu ya Kristo kwa kufanikisha ujenzi wa zahanati ya kisasa katika kijiji cha Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani.

 

Mganga huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa zahanati hiyo, pamoja na kuwapongeza amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yote kwa lengo la kuwezesha kila kijiji kiwe na zahanati  kila kata na kila wilaya kuwa na hospitali.

 

Zahanati hiyo ya DA.MA Africa imejengwa kwa ufadhili wa wakristo wa Italia chini ya usimamizi wa raia kutoka Italia, Germano Frioni.

 

 

Comments are closed.