ZAIDI YA WAHAMIAJI 200 WAANGAMIA LIBYA

ZAIDI YA WAHAMIAJI 200 WAANGAMIA LIBYA

Like
220
0
Friday, 28 August 2015
Global News

ZAIDI ya watu mia mbili wanahofiwa kufariki baada ya boti mbili iliyokuwa imebeba wahamiaji haramu kuzama katika eneo la Zurawa pwani ya Libya.

Mamia ya wahamiaji wengine wameokolewa na wanamaji wa Libya usiku wa kuamkia leo.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja Libya haijakuwa na serikali thabiti na sehemu kubwa ya nchi hiyo inathibitiwa na wanamgambo wa Kiislamu, na walanguzi wa watu wanatumia nafasi hiyo kusafirisha watu kimagendo hadi Ulaya.

Comments are closed.