ZAIDI YA WATU 50 WAHOFIWA KUFA MAJI LIBYA

ZAIDI YA WATU 50 WAHOFIWA KUFA MAJI LIBYA

Like
195
0
Friday, 04 September 2015
Global News

ZAIDI ya watu hamsini hawajulikani waliko baada ya meli walimokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Libya.

 

Msemaji wa shirika la kimataifa ya uhamiaji amesema kuwa wahamiaji wengine waliokuwa kwenye meli hiyo waliokolewa na wanajeshi wa majini wa Italia na wamepelekwa kisiwa cha Lampedusa.

 

Mwili wa mhamiaji mmoja pia uliopolewa baharini na kupelekwa katika kisiwa hicho.

 

KWINGINEKO, INAELEZWA kuwa Watu 1,000 nchini Sierra Leone wamewekwa kwenye karantini baada ya kugunduliwa kuwa mwanamke wa umri wa miaka 67 alifariki kutokana na Ebola.

 

Hilo limejiri siku tano tu baada ya kuanza kwa hesabu ya wiki sita iliyolenga kutangaza taifa hilo kuwa halina Ebola.

 

Watu Zaidi ya 11,000 wamefariki tangu kuanza kwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone, Guinea na Liberia.

Comments are closed.