ZARIF AKOSOA MAOMBI YA KUMTAKA RAIS BASHAR KUJIUZULU

ZARIF AKOSOA MAOMBI YA KUMTAKA RAIS BASHAR KUJIUZULU

Like
229
0
Tuesday, 08 September 2015
Global News

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, ameyakosoa vikali madai ya kumtaka Rais Bashar al-Assad ajiizulu akisema kuwa wanaoyatoa ndio wenye dhamana ya umwagikaji damu nchini Syria.

Akizungumza mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Hispania aliye ziarani nchini Iran José Manuel Margallo,  waziri  Zarif amesema kuwa hakuna suluhisho la kijeshi kwa mzozo wa Syria na kwamba hakuna anayeweza kulazimisha matakwa yake kwa watu wa Syria.

Ingawa Zarif hakuitaja nchi yoyote kwa jina, lakini uwezekano mkubwa ni kuwa amezikusudia nchi za Uturuki na Saudi Arabia, ambazo zimerejea wito wao wa kumtaka Assad ajiuzulu.

Comments are closed.