ZIARA YA RAIS WA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA VIETNAM KUANZA MACHI 9 NCHINI

ZIARA YA RAIS WA JAMHURI YA KISOSHALISTI YA VIETNAM KUANZA MACHI 9 NCHINI

Like
288
0
Friday, 04 March 2016
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Truong Tan Sang anatarajiwa kufanya ziara rasmi Tanzania tarehe 9 Machi mwaka huu na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam.  

Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza uhusiano baina ya Vietnam na Tanzania ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake pamoja na ‎Kufungua maeneo mapya ya Ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Vietnam.

Hiyo ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo Barani Afrika tangu aingie madarakani mwaka 2011, ambapo nchi nyingine anayotarajia kuitembelea ni Msumbiji.

Comments are closed.