ZIDANE AKABIDHIWA MIKOBA YA BENITEZ KUINOA REAL MADRID

ZIDANE AKABIDHIWA MIKOBA YA BENITEZ KUINOA REAL MADRID

Like
335
0
Tuesday, 05 January 2016
Slider

Zinedine Zidane achukua nafasi ya Rafael Benitez kuinoa Real Madrid.

Rafael Benitez ametimuliwa katika nafasi ya kuwa meneja wa klabu ya Real Madrid baada ya kushika hatamu ya uongozi katika kipindi cha miezi 7 kabla kibarua kuota nyasi.

Mhispania huyu, Benitez, 55 ameanguliwa kwenye nafasi hiyo baada ya kikao cha bodi ya klabu hiyo kukutana na kufikia maamuzi hayo.

Zidane, 43, amepandishwa kutoka kwenye nafasi yake ya awali ambapo alikuwa anakinoa kikosi B cha klabu ya Real Madrid

 

Mfaransa huyu ambae pia ni nyota wa zamani wa Real Madrid amesema kuwa atawekeza nguvu zake kwa kujitolea kwa moyo mmoja kufanya kazi na kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.

 

Real Madrid ilishuka dimbani kukipiga na Valencia mchezo uliomalizika kwa sare ya magoli 2-2 huku ukiwa mchezo wa mwisho kwa kikosi cha Real Madrid chini ya Benitez

Comments are closed.