MASHIRIKA ya kutetea maslahi ya wanyama nchini Zimbabwe yameonesha kushangazwa na hatua ya nchi hiyo kuuza Tembo kwa madai kwamba inahitaji fedha kwaajili ya kukabiliana na uwindaji haramu.
Waziri wa mazingira nchini humo amesema kuwa tembo hao walisafirishwa kwa ndege hadi China kwenye ndege binafsi ya mizigo huku wahifadhi wa wanyama wanasema wanyama hao wanahitaji uangalifu wa miaka kadhaa kutoka kwa wazazi wake.
Tembo hao wataishi katika mbuga ya wanyama karibu na mji uliopo kusini mwa china– Guangzhou wakati taarifa zinaonesha kuwa wanyama katika mbuga hiyo wanateswa na kuwekwa katika mzingira mabaya.