ZIMBABWE: MSHINDI WA MASHINDANO YA UBAYA KUKUTANA NA UPINZANI MKUBWA

ZIMBABWE: MSHINDI WA MASHINDANO YA UBAYA KUKUTANA NA UPINZANI MKUBWA

Like
670
0
Friday, 13 November 2015
Entertanment

Muandaaji wa mashindano ya Ubaya nchini Zimbabwe maarufu kama Mr Zimbawe bwana David Machowa amesema kwa mara ya kwanza mshindi wa muda wote wa mashindano hayo bwana William Masvinu anatarajiwa kukutana na upinzani mkali kufuatia kuongezeka kwa idadi ya washiriki.

Tangu mwaka 2012 Masvinu amekuwa akitwaa taji hilo ambapo idadi ya washiriki walikuwa watano na alifanikiwa kubeba $100 na nafasi ya kulala katika moja ya hoteli za Harare akiwa amelipiwa kila kitu.

Waandaji wa mashindano hayo wameongeza kitita cha fedha hadi kufikia $1,000 kwa mshindi atakaepatikana mwaka huu ambapo kilele chake kinarajiwa kufanyika mwezi wa November.

Akiongeza kuhusu mipango yake ya kupanua shindano hilo bwana David Machowa amesema anaangalia uwezekano wa kutanua shindano hilo katika mataifa ya kusini mwa Afrika lakini pia anasema ameamua kufanya hivyo ili kuwafanya watu wajivunie jinsi walivyoumbwa na kuacha kujisikia vibaya

Comments are closed.