ZIMBABWE: MUUAJI WA SIMBA CECIL KUTOSHITAKIWA

ZIMBABWE: MUUAJI WA SIMBA CECIL KUTOSHITAKIWA

Like
254
0
Tuesday, 13 October 2015
Global News

WAZIRI wa Mazingira wa Zimbabwe Oppah Muchinguri amesema kuwa daktari wa meno ambaye alisababisha hali ya taharuki baada ya kumuua Simba mmoja mashuhuri nchini Zimbabwe hatashtakiwa kwa kuwa alikuwa na kibali cha kuwinda.

Daktari huyo anayefahamika kwa jina la Walter Palmer alikubali kumuua Simba aitwaye Cecil lakini alikana kutekeleza shughuli za uwindaji kinyume cha sheria.

Awali Waziri huyo alitaka Palmer afunguliwe mashtaka ya kumuua mnyama huyo lakini baadaye ilibainika kuwa hakuna sheria iliyovujwa katika mauaji ya Simba huyo.

Comments are closed.