ZITTO AMTAKA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KUJIUZULU

ZITTO AMTAKA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KUJIUZULU

Like
273
0
Monday, 02 February 2015
Local News

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini mheshimiwa ZITTO KABWE amemtaka waziri wa maliasili na Utalii ambaye pia ni mbunge wa Singida mheshimiwa LAZARO NYALANDU kujiuzuru endapo atashindwa kutekeleza agizo la utoaji wa tangazo katika gazeti la serikali juu ya tozo na mapato yatokanayo na wageni wanaolala katika hoteli za kitalii zinazozunguka hifadhi za Taifa hadi ifikapo leo jioni.

Mheshimiwa ZITTO ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia taarifa za utekelezaji wa mikakati mbalimbali zilizotolewa na kamati ya Ardhi, maliasili na mazingira pamoja na kamati ya kilimo, mifugo na maji katika kipindi cha kuanzia Januari mwaka jana hadi Januari mwaka huu.

Mbali na hayo amesema kwamba kushindwa kutolewa mapema na kwa muda muafaka kwa tangazo hilo kumeisababishia serikali hasara kubwa ya kupotea kiholela kwa mapato ya Taifa na kuongeza kuwa hali hiyo inaonesha utekelezaji mbovu kwa wizara husika.

 

Comments are closed.