ZLATAN IBRAHIMOVIC AFUNGIWA MECHI MBILI NA KAMATI YA MAADILI UFARANSA

ZLATAN IBRAHIMOVIC AFUNGIWA MECHI MBILI NA KAMATI YA MAADILI UFARANSA

Like
291
0
Friday, 20 February 2015
Slider

Mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint-Germain Zlatan Ibrahimovic amefungiwa michezo miwili katika mashindano ya ndani ya ligi ya Ufaransa (LFP).

Mshambuliaji huyo ambae ni raia wa Sweden amepewa adhabu hiyo  na kamati ya maadili ilpokutana kujadili hatima yake na kukutwa na hatia ya kufanya madhambi

Kutokana na adhabu hiyo Ibrahimovic ataikosa mechi na Monaco siku jumapili ya tarehe moja mwezi wa tatu kwenye robo fainali ya michuano ya ligi nchini Ufaransa.

Adhabu hiyo huenda ikaleta madhara kwa klabu ya PSG kutokana na umuhimu wake kwa kuungoza na magoli 17 kwenye msimu huu akifuatiwa na Edinson Cavani.

Comments are closed.