ZOEZI la kuhesabu kura linaendelea visiwani Zanzibar baada ya uchaguzi wa marudio uliofanyika jana.
Imeelezwa kwamba idadi ndogo ya wapiga kura imejitokeza kushiriki katika uchaguzi huo ambao ulisusiwa na baadhi ya vyama vikuu vya upinzani.
Nchi nyingine za Afrika ambazo zimefanya Uchaguzi jana ni pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Niger na nchi ya Cape Verde ambapo tayari chama kikuu cha upinzani nchini humo MPD kimeshinda baada ya uchaguzi wa jana kwa zaidi ya asilimia 53 huku mkuu wa chama tawala PAICV Janira Hopfer Almada amekubali kushindwa baada ya asilimia 90 ya matokeo.