ZOEZI LA KURA ZA MAONI KUANZA LEO CHADEMA

ZOEZI LA KURA ZA MAONI KUANZA LEO CHADEMA

Like
279
0
Monday, 20 July 2015
Local News

BAADA ya mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania uteuzi wa ndani wa nafasi ya ubunge kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo kumalizika, imeelezwa kuwa zoezi la kura za maoni linaanza leo hadi julai 25 mwaka huu.

 

Katika hatua hiyo kila uongozi wa kanda umepanga ratiba yake ya kura za maoni katika majimbo mbalimbali kwa kuzingatia kuwa zoezi hilo limeagizwa kufanyika na kumalizika ndani ya siku 6 katika majimbo yote ya uchaguzi nchi nzima.

 

Hata hivyo  taarifa kutoka Idara ya Habari ya chama hicho,  zimebainisha kuwa kupitia mchakato huo chama kitapata wagombea makini wa nafasi ya ubunge ambao watakihakikishia chama hicho ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi  Oktoba 25 mwaka huu.

 

Comments are closed.