MAREKANI: TRUMP APETA MICHIGAN NA MISSISSIPPI

MAREKANI: TRUMP APETA MICHIGAN NA MISSISSIPPI

Like
244
0
Wednesday, 09 March 2016
Global News

MGOMBEA Urais wa Marekani anayeongoza katika chama cha Republican Donald Trump, amejiongezea ushawishi kama mgombea mkuu kufuatia ushindi wake katika majimbo ya Michigan na Mississippi.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa wamesema kuwa ushindi huo mara mbili umezima uvumi wa mwishoni mwa wiki kuwa kampeni yake Trump ilikuwa imepoteza kasi.

Baada ya kupata ushindi huo, Trump amesema kuwa anakiongezea umaarufu chama cha Republican ingawa Mshindani wake mkuu Seneta Ted Cruz naye amepata ushindi katika jimbo dogo la Idaho.

Comments are closed.