17 WAZAMA BAHARINI SYRIA

17 WAZAMA BAHARINI SYRIA

Like
280
0
Monday, 28 September 2015
Global News

KIASI cha raia 17 wa Syria wamezama katika bahari ya Aegean baada ya kuondoka Uturuki wakielekea Ugiriki.

Takriban wahamiaji wengine 20 kutoka Syria wameokolewa na maafisa wa Uturuki baada ya boti yao kuzama na Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti hapo jana kuwa miongoni mwa waliokufa maji ni watoto watano.

Boti hiyo ilikuwa imewabeba wahamiaji 37 na kwa mujibu wa shirika la kimataifa la kushughulikia wahamiaji IOM, zaidi ya wahamiaji laki 350,000 wengi wao kutoka Syria wameingia Ugiriki mwaka huu kupitia Uturuki.

Comments are closed.