AZAM BINGWA CECAFA KAGAME CUP 2015

AZAM BINGWA CECAFA KAGAME CUP 2015

Like
297
0
Monday, 03 August 2015
Slider

Hongera Azam Fc kwa kutwaa ubingwa  Cecafa kagame Cup kwa mwaka 2015 wakiwa na historia ya kutoruhusu nyavu zake kutikiswa huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa wanalambalamba kutwaa taji hili.

Azam wametwaa taji hilo hapo jana katika uwanja wa taifa baada ya kuichapa timu ya Gor Mahia ya Kenya kwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali

Ushindi huo wa wanalambalamba ni matunda ya magoli yaliyofungwa na washambuliaji wake John Bocco na Kipre Tchetche aliyepiga mpira wa adhabu nakuzama moja kwa moja nyavuni.

 

Katika mchezo wa awali KCCA ya Uganda iliichapa Al Khartoum 2-1 na kutwaa nafasi ya Mshindi wa 3 wa Kagame Cup.

Bao za KCCA zilifungwa na Michael Birungi na Muzamir Mutyaba na lile la Al Khartoum kuingizwa na Ousmaila Baba.

Azam FC kwa kuwa Mabingwa wa Kagame Cup wamezoa Kombe pamoja na kitita cha Dola 30,000 huku Gor Mahia wakipata Dola 20,000 na KCCA Dola 10,000

 

 

Comments are closed.