30% YA WATU DUNIANI VIBONGE NA WANAVITAMBI

30% YA WATU DUNIANI VIBONGE NA WANAVITAMBI

Like
406
0
Thursday, 20 November 2014
Local News

gharama za unene wa kupitiliza duniani ni  sawa na utumiaji wa bidhaa za tumbaku ukiwemo uvutaji wa sigara au sawa na gharama za vita na kubwa kuliko unywaji wa pombe au mabadiliko ya tabia nchi.

Watafiti wanasema Watu wapatao bilioni 2.1 – kiasi cha asilimia 30% ya idadi ya watu duniani- wana uzito wa kupita kiasi au wana vitambi.

Wamesema hatua ambazo zinatakiwa kutumiwa ili kutatua tatizo hili ni mtu binafsi kuwajibika kwa ajili ya afya yake. Ripoti hiyo inasema kuna “gharama kubwa za kiuchumi”, na uwiano unaweza kukua kufikia karibu nusu ya idadi ya watu duniani ifikapo mwaka 2030.

Gharama ya fedha kwa wenye vitambi inazidi kuongezeka- kwa huduma za afya na kwa upana zaidi katika uchumi. Kwa kusababisha maradhi, kitambi kina madhara katika utendaji wa kazi na kupotea kwa tija.

Comments are closed.