HATIMAE KENYATTA AIKABILI ICC LEO NA KUWEKA REKODI

HATIMAE KENYATTA AIKABILI ICC LEO NA KUWEKA REKODI

Like
327
0
Wednesday, 08 October 2014
Global News

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko Hague, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.

Yeye ni kiongozi wa kwanza wa taifa kuwasili mbele ya mahakama hiyo.

Kenyatta amefika mbele ya mahakama hiyo baada ya waendesha mashtaka kuishutumu serikali ya Kenya kukata kuwasilisha ushahidi muhimu.

Kenyatta amekanusha madai ya kupanga na kufadhili ghasia za kikabila nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka 2007/2008.

Kikao cha leo kitatathmini ombi la upande wa mashitaka la kutaka kuahirishwa kwa kesi hiyo hadi pale serikali ya Kenya itakapoikabidhi mahakama hiyo ushahidi unaohitajika kuhusiana na mali ya Rais Kenyatta.

Upande wa utetezi nao unataka kesi hiyo ifutiliwe mbali ukisema kuwa upande wa mashitaka hauna ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea.

Kiongozi wa mashitaka Fatou Bensouda, amewasili mahakamani akisema kesi hiyo iko katika awamu muhimu sana.

Kenyatta ameamua kukaa kimya akimtaka wakili wake kuongea kwa niaba yake.

 

Comments are closed.