MADEREVA wa Pikipiki maarufu Bodaboda, wameilalamikia Serikali kwa kutowatengea maeneo maalumu ya kupaki pikipiki zao katika kituo kipya cha mabasi cha Ubungo kilichopo Kata ya Sinza C.
Wakizungumza na Efm Jijini Dar es salaam Madereva hao wamesema kuwa ujio wa kituo hicho imekuwa ni kero kwani hawana sehemu maalumu ya kupaki na wamekuwa wakiondolewa na vijana wa Ulinzi Shirikishi na kutozwa pesa isio kuwa na kiwango na watu wasiojulikana.
Wamebainisha kuwa inapaswa Serikali iwatambue na kuwajali kuwa nao wana mchango katika kukuza pato la taifa pamoja na kuondokana na adha ya kukosa ajira kwa vijana.