Kamati ya maamuzi ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF) imewapa muda wa siku tano mpaka siku ya jumamosi ya tarehe nane mwezi wa kumi na moja mwaka huu kutoa tamko rasmi juu ya uaandaaji wa michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2015
Morocco walipewa kibali cha kuandaa michuano hiyo lakini kutokana na hofu ya ugonjwa wa Ebola iliwaomba CAF waisogeze mbele au kuahirisha kabisa michuano hiyo iliyopangwa kuanza tarehe 17 mwezi januari mpaka Februari 8 mwaka 2015.
Wakati huohuo CAF imewaomba nchi wanachama wanaotaka kuandaa michuano hiyo endapo nchi ya Morocco itaamua kujitoa waweze kuwasilisha maombi yao siku hiyohiyo ya tarehe nane mwezi wa kumi na moja ili wafikie maamuzi tarehe kumi na moja mwezi wa kumi na moja mwaka 2015.
Nchi mbalimbali zimeshaanza kuonyesha nia ya kuandaa ikiwemo Nigeria ambayo pia ilikumbwa na ugonjwa wa Ebola huku Afrika ya Kusini kupitia Rais wa shirikisho la soka nchini humo Danny Jordan ilijitoa katika kinyang’anyiro cha kuandaa.