POLISI nchini Israel wamepambana na vijana wa Kipalestina waliokuwa wakirusha mawe ndani ya uwanja wa msikiti wa Al-Aqsa leo baada ya makundi ya Wayahudi wenye msimamo mkali kutangaza mipango ya kuzuru eneo hilo licha ya wiki kadhaa za hali ya wasi wasi.
Ziara hiyo iliyopangwa na kundi la Wayahudi ikiwa ni pamoja na wanasiasa wa siasa za kizalendo zaidi ilikuwa ifanyike wiki moja baada ya jaribio la mauaji dhidi ya mmoja kati ya wanaharakati maarufu lililofanywa na Mpalestina aliyekuwa na silaha na kusababisha Israel kulifunga eneo hilo, ambalo ni takatifu kwa Wayahudi na Waislamu.
Ghasia hizo zimezuka wakati waandamanaji waliporusha mawe na vitu vinavyoripuka baada ya polisi kufungua lango la Mughrabi kwa watu hao wanaotaka kuzuru eneo hilo.