ZAIDI ya Wahudumu 400 wa Afya wanaowatibu Wagonjwa wa maradhi ya ugonjwa wa Ebola katika Kliniki moja nchini Sierra Leone wamegoma.
Wahudumu hao wakiwemo wauguzi na wafanyakazi wengine wanagoma kushinikiza kuwalipa Dola Miamoja kila wiki kwa kuhatarisha maisha yao kutokana na kuwashughulikia wagonjwa wa hao.
Kliniki hiyo iliyo mjini Bandajuma karibu na eneo la Bo, ni kliniki pekee ambayo wagonjwa wa Ebola wanatibiwa Kusini mwa Sierra Leone.
Kwingineko nchini Mali, muuguzi mmoja pamoja na mgonjwa aliyetibiwa na muuguzi huyo wamefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola.