SERIKALI imeagiza wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kushirikiana ipasavyo na wizara ya fedha katika utendaji wao wa kazi ikiwemo uingizwaji na uagizwaji wa dawa ili kuhakikisha kuwa zinapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa dawa katika hospitali zote nchini.
Agizo hilo limetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri mkuu mheshimiwa MIZENGO PINDA wakati akijibu swali la mheshimiwa ANTON MBASA aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kuhakikisha tatizo la upungufu wa dawa katika hospitali zote nchini linatatuliwa.