WAJERUMANI 550 KUJIUNGA NA WANAMGAMBO WENYE ITIKADI KALI SYRIA NA IRAQ

WAJERUMANI 550 KUJIUNGA NA WANAMGAMBO WENYE ITIKADI KALI SYRIA NA IRAQ

Like
546
0
Monday, 24 November 2014
Global News

MKUU WA SHIRIKA la kitaifa la ujasusi nchini Ujerumani HANS GEORGE MAASSEN amesema Maafisa wa Usalama nchini humo wanawafahamu watu 550 kutoka Ujerumani ambao wamesafiri kuelekea Syria na Iraq kujiunga na makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali na kiasi cha watu sitini kati yao wameshakufa.

Akihojiwa na gazeti linalochapishwa kila Jumapili la Welt am Sontag, Bwana MAASSEN amesema watu hao Sitini wameuawa au kujitoa Muhanga katika mashambulizi.

Maafisa wa usalama Ujerumani na nchi nyingine za bara la Ulaya wamekuwa na wasiwasi na ongezeko la raia wake wanaojiunga na makundi yenye itikadi kali na ambao wanarejea nyumbani na kuongeza hatari ya kiusalama.

 

Comments are closed.