MAKUNDI YA KUTETEA Haki za Binaadamu yamesema kuwa Mapendekezo ya Serikali ya Kenya, kuimarisha Sheria za Usalama yanahatarisha nchi hiyo kuwa Dola inayotawaliwa na polisi.
Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya mashirika ya kutetea haki za binaadamu ya Kimataifa, HUMAN RIGHTS WATCH na AMNESTY International, iwapo marekebisho ya sheria za usalama yanayopendekezwa yatapitishwa, yatazibana haki za watu waliokamatwa na watuhumiwa na kudhibiti Uhuru wa kujieleza na kukusanyika.
Mapendekezo hayo ambayo huenda yakapitishwa na wabunge wa Kenya kabla ya Mapumziko ya Sikuu Kuu ya Krismasi, yanajumuisha kuongeza muda wa polisi kuwazuwia washukiwa wa ugaidi kutoka siku 90 hadi siku 360 na kuongeza muda wa vifungo vyao na kuongeza madaraka ya udukuzi wa mawasiliano.