Pakistan imeingia siku yake ya pili ya maziko na maombolezo, baada ya kundi la wanamgambo wa Taliban kuivamia Shule moja ya Kijeshi na kuwauwa watu 141, wengi wao watoto.
Mashambulizi hayo ya kikatili zaidi kuwahi kutokea katika siku za karibuni, yamelaaniwa na viongozi na watu kadhaa mashuhuri duniani.
Aidha kundi la Taliban katika nchi jirani ya Afghanistan limeyaita mauaji hayo kuwa ni ya kinyama na yasiyo na uhalali wowote kidini. Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif, ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa