SHIRIKA la Junior Archvment kwa kushirikiana na Citi Benki wamewapongeza vijana wajasiriamali walioshinda katika shindano la bidhaa bora lililofanyika jijini Dar es salaam kwa lengo la kumtafuta mshindi wa bidhaa bora atakayewakilisha katika shindano la Ujasiriamali Afrika.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi watatu kati ya makundi 13 walioshiriki, mkurugenzi wa shirika lisilo la serikali la Junior archievement Maria Ngowi amesema shirika hilo limekuwa likidhaminiwa na CITI Benki ili kuweza kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri mdogo ili waweze kumiliki uchumi binafsi.