Klabu ya West Bromwhich Albion nimemfungashia virago kocha Alan Irvine ikiwa ni miezi saba tu toka apewe mikoba ya kukinoa kikosi hicho kinachokipiga katika uwanja wa Hawthorns.
Irvine raia wa Scotland mwenye umri wa miaka 56 aliteuliwa kukinoa kikosi cha WBA baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Pepe Mel kutimuliwa, amekuwa akipata matokeo mabovu na kuwaacha klabu hiyo katika nafasi ya 16 ndani ya msimu wa ligi kuu nchini England.
West Brom inataraji kusafiri kwenda jijini London kumenyana na klabu ya West Ham United itaongozwa na makocha Robby Kelly na Keith Downing waliokuwa wsasaidizi wa Irvine.
Makocha mbalimbali wameanza kuhusishwa na kuchukua mikoba ya Irvine akiwemo Tim Sherwood aliyekuwa kocha wa Spurs pamoja na Tony Pulis aliyewahi kuvinoa vikosi vya Stoke City na Crystal Palace.