AC MILAN YATWAA UBINGWA DUBAI CHALLENGE BAADA YA KUILAZA 4-2 REAL MADRID

AC MILAN YATWAA UBINGWA DUBAI CHALLENGE BAADA YA KUILAZA 4-2 REAL MADRID

Like
445
0
Wednesday, 31 December 2014
Slider

Klabu ya soka ya AC Milan imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Dubai Challenge kwa kuitandika mabingwa wa dunia kwa upande wa klabu na barani Ulaya, Real Madrid magoli 4-2.

Magoli ya AC Milan yalifungwa na wachezaji Stephen El Shaaraway aliyefunga magoli mawili, Jeremy Menez na Giampaolo Pazzini huku kwa upande wa Real Madrid yakifungwa na mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Karim Benzema.

MILAN2 MILAN3

Milan inayonolewa na kocha Phillipo Inzaghi aliyewahi kucheza chini ya kocha wa sasa wa Real Madrid, Carlo Ancelloti kipindi wapo AC Milan ilionyesha kandanda safi n akuendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika michezo mitatu iliyopita ambapo walikutana na klabu za Napoli na Juventus.

Kipigo hiki hakijaathiri rekodi ya klabu ya Real Madrid ya kushinda michezo 22 mfululizo kwasababu hii ilikiuwa ni mechi ya kirafiki na rekodi hiyo inasimama katika mechi za ushindani tu kama La Liga, Klabu bingwa Ulaya, Kombe la mfalme na mengineyo.

Comments are closed.