WAZIRI wa maji Jumanne Maghembe ametoa siku 90, kwa mkandarasi Megha Engineering Infrastructure Limited anaesambaza bomba la maji mradi wa Mlandizi Kimara kufanikisha mradi huo na kupeleka ripoti ya maradi kwenye Mamlaka ya maji safi na maji taka (Dawasco), kwalengo la kupata tathimini ya mradi.
Ametoa agizo hilo jana akiwa mkoani Pwani wakati akikagua miradi minne ya Dawasco, yakusambaza maji Ruvu juu na Ruvu Chini kufikisha Jijini Dar es Salaam.
Aidha amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Arcado Mutalemwa kuhakikisha pampu zilizokwama bandarini zinafika leo na kufungwa kesho siku ya Alhamisi.