KIONGOZI wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Uganda, Lord’s Resistance Army, LRA amekabidhiwa kwa wawakilishi wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC, na sasa ameshawasili mjini The Hague ambako atafunguliwa kesi.
Kiongozi huyo Dominic Ongwen atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Kundi la kigaidi la LRA kwa muda mrefu limekuwa linafanya vitendo vya kinyama katika nchi za Afrika mashariki na kati. Ongwen alijisalimisha mwenyewe kwa majeshi ya Marekani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati,yanayosaidiana na majeshi ya Umoja wa Afrika katika kuwasaka magaidi wa LRA.