SERIKALI ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC ,imesema kwamba takriban watu 11 wakiwemo raia wameuawa mjini Kinshasa tangu vurugu zilizosababishwa na mswada tatanishi wa uchaguzi kuanza Jumatatu.
Msemaji wa Serikali, Bwna Lambert Mende amesema Mswada huo umetajwa na wanasiasa wa upinzani kama mapinduzi ya kikatiba wakisema utamfanya Kabila kujiongeza muda madarakani kwa miaka mingine mitatu.
Mswada huo unajadiliwa na baraza la seneti huku viongozi wa upinzani wakiitisha maandamano mengine hii leo kuupinga mswada huo.