UMOJA wa Ulaya umesema leo kuwa mahakama nchini Misri imekiuka majukumu yake ya kimataifa kuhusu haki za binadamu kwa kuwahukumu watu 183 adhabu ya kifo jana kwa kuwauwa polisi 13.
Idara ya mambo ya kigeni ya Umoja wa Ulaya imesema katika taarifa yake kuwa uamuzi uliotolewa na mahakama ya Misri kuwahukumu washitakiwa 183 adhabu ya kifo kufuatia kesi ya jumla ni ukiukaji wa majukumu ya Misri ya haki za binadamu.
Hukumu iliyotolewa jana , ambayo inaweza kukatiwa rufaa , imekuja baada ya hukumu za awali kupelekwa kwa mufti, ambaye ni afisa wa serikali ya Misri anayetafsiri sheria za Kiislamu, kwa ajili ya kuidhinishwa.